VIDEO:DADA ALIVYOVULIWA NGUO KWA KUVAA NUSU UCHI MWEZI WA RAMADHANI

Video
SOMA MPAKA MWISHO AMBAPO KUNA VIDEO ZOTE ZA TUKIO HILO

Waumini wa dini ya Kiislamu wanalazimika kwa mujibu wa maamrisho ya dini yao kufunga.Hii
huenda pamoja na kufuatilia kwa karibu zaidi mafunzo na maamrisho ya dini yao, ikiwa pamoja na kuwasaidia wasiojiweza na kujitahidi kufanya mema na kuachana na maovu.

Kufunga katika mwezi huu ambapo Waislamu waliteremshiwa na Mola kitabu chao kitukufu cha Quran ni
moja ya nguzo tano za dini hiyo.

Waislamu hufunga kuanzia muda mfupi kabla ya kuchomoza isha za jua kutoka hadi pale linapotua.

Katika funga yao, Waislamu hutakiwa kujiepusha na mengi ikiwa ni pamoja na
kula, kunywa, kuvuta sigara na hata kusema uongo au kufanya vitendo vya
mahaba hata na wanandoa wenzao.

Kwa Waislamu wengi wa Tanzania funga huchukua kati ya saa 14 na saa 14 na dakika 30 kwa
kutegemea funga hiyo unaifanyia sehemu gani ya nchi, lakini wapo wenzao
katika baadhi ya nchi ambako usiku huwa mkubwa kutokana na majira ya
hali ya hewa na hufunga kwa hadi saa 20.

Katika mwezi huu, Wazanzibar na wageni hutakiwa kuzifuata sheria na taratibu
zilizowekwa kisheria na wanaozikiuka hupata adhabu ya kifungo cha mwaka
mmoja usiokuwa na hata siku moja ya msamaha.

Adhabu hii huwakuta watu wazima na wenye akili timamu (bila ya kujali umri).Hii
ni kusema anayekamatwa anakula siku ya tatu ya Ramadhani huenda jela
hadi siku ya tatu ya Ramadhani ya mwakani kwa sababu ya kuonyesha jeuri
kwa dini ya Kiislamu na kuchezea hisia za Waislamu.

Mara chache huwapo adhabu ya faini kwa makosa haya.Uvaaji wa mavazi,Kwa
miaka mingi Zanzibar imekuwa na mwongozo wa mavazi anayotakiwa mtu
kuvaa hadharani, lakini sheria hii ambayo imekuwa ikifumbiwa macho
kutokana na kile kinachoelezwa kama utandawazi husimamiwa kwa nguvu
ukifika mwezi wa Ramadhani.

Kwa mfano, kitendo cha kuvaa nguo fupi sana mwanamke na kuwa mgongo wazi au kuvaa nguo nyepesi
inayoonyesha mambo hadharani, kwa mujibu wa sheria za mavazi ya
Zanzibar, ni kosa la jinai. Wanaofanya hivyo wanapokamatwa husukumwa
jela au kuchapwa viboko.

Katika miaka ya nyuma, watalii waliofika Zanzibar na ‘vinguo’ vifupi walilazimishwa kununua kanga au
vitenge na kufunika vizuri maumbile yao. Waliokataa kufanya hivyo
walitakiwa kurudi walikotoka kwa sababu Zanzibar haikuwa tayari kuona
watu wanakwenda nusu au robo uchi hadharani.

Sheria hii ilikuwapo tangu wakati wa utawala wa Sultani na ilisimamiwa kwa nguvu
zaidi wakati wa utawala wa Rais wa kwanza wa Zanzibar baada ya Mapinduzi
ya 1964, Abeid Amani Karume mpaka kifo chake mwaka 1972.

Karume alikuwa akisema mtu yupo huru kwenda uchi nyumbani kwake, lakini
akifanya katika barabara za Unguja na Pemba atapelekwa jela
akafundishwe kuvaa virago vya gerezani.

Alisema anayependa kuonyesha uzuri wa umbo lake afanye kwenye kioo nyumbani kwake na sio katika barabara za Zanzibar.,Karume alivyodhibiti uvaaji,Siku
moja balozi mmoja wa Kiingereza alifika Ikulu ya Zanzibar kuonana na
Mzee Karume. Lakini mara tu alipomuona, Rais Karume alirudi ofisini
kwake na kuwaambia maofisa wake wamwambie balozi aende kuvaa nguo zenye
heshima na stara kwa vile Zanzibar sio nchi ya watu wanaotembea uchi.

Katika mkasa wa pili ulioonyesha namna ambavyo Rais Karume alivyokataa wageni
na hata viongozi kuchezea au kukebehi utamaduni wa Zanzibar ni pale Rais
wa Liberia, William Tubman alipokuwa afike Zanzibar alipofanya ziara ya
Tanzania mwaka 1964.

Siku chache kabla ya Tubman kufika Zanzibar, Karume alitembelewa Ikulu na maofisa wa itifaki wa
Liberia kumweleza namna mzee Karume alivyotakiwa kumpokea kiongozi huyo
wa Liberia na matayarisho gani amfanyie ili ziara yake iwe ya mafanikio.

Rais Karume alisikiliza kwa utulivu, alitakiwa avae suti nyeusi na afunge
tai shingoni na maneno gani atumie kumkaribisha na kwamba amtayarishie
kinywaji aina ya whisky wakati wa chakula na mazungumzo.

Baadaye Karume aliangua kicheko na kuwaambia maofisa wa itifiki wa Liberia na
Tanzania, kwamba kama Tubman aliamua kutembelea Zanzibar aonyeshe
heshima na adabu na lazima avae kanzu na koti, kofia ya baraghashia na
viatu vya makubazi.

Vilevile aliwaambia bosi wao afikapo Zanzibar anywe maji ya madafu na kama hakuwa tayari kufanya
hivyo asifike Zanzibar. Wakati alipokuwa akitamka hayo Karume
alikwishatoa maelekezo kwa maofisa wake kwenda kumnunulia Tubman kanzu,
kofia na viatu vya makubazi.

Balaa kubwa lilizuka na mzee Karume alikubali baadaye yaishe na kila mmoja avae vazi lake,
lakini hata Rais Tubman hakuruhusiwa kwenda Zanzibar na pombe.

Tubman alifika Zanzibar akiwa amevaa suti na mzee Karume alimpokea akiwa
amevaa kanzu maridadi. Hiyo ndiyo Zanzibar ilivyokuwa hapo zamani na
hasa katika mwezi wa Ramadhani.Tahadhari muhimu

Sikuhizi hali imebadilika, lakini viongozi wa Zanzibar kila ikifika mwezi
wa Ramadhani huwataka wenyeji na wageni, wakiwamo watalii kuuheshimu
mwezi huo kwa kufuata sheria na maelekezo yanayotolewa na Serikali.

Haya kuwatahadharisha wageni, wakiwamo ndugu zetu wa Kikristo waliopo
Bara wanaofika Zanzibar wakati wa mwezi huo iwe kwa kazi au matembezi
kwamba kama wakifanya ‘maraha’ au wakila, kunywa au kuvuta sigara
hadharani wanaweza kujikuta katika balaa.

Kila nchi ina sheria zake na zinapaswa kuheshimiwa. Katika baadhi ya nchi ni kosa la
jinai kuvaa hijabu na sheria hizo anayezivunja hukiona cha mtema kuni.

Kwa hiyo, isiwe nongwa kwa Zanzibar kuwa na sheria zake na anayeona tabu ni
vyema akavumilia au aamue asifike Zanzibar, hasa wakati wa mwezi huu
mtukufu.

Nchi nyingi za Magharibi huwaonya raia zake wanaotembelea nchi za Kiislamu na hasa Saudi Arabia na nchi za Ghuba kuwa na hadhari ya kutokula au kunywa hadharani wakati wa mwezi huu
kwani kufanya hivyo kutawaweka matatizoni.

Ni vizuri pia zikafanya hivyo kwa wale wanaofika Zanzibar wakati huu kwa sababu
mbali ya polisi kuwa ndio msimamizi wa sheria hizi, wakati fulani hata
wananchi wenye hasira huchukua sheria mkononi.

Mara nyingi imetokea watu wanaokula hadharani au kuvaa nguo fupi kwenye
maeneo ya wazi, hasa mwezi wa Ramadhani kuchapwa na hata kuumizwa na
watu wenye hasira ambao huona dini yao inabughudhiwa.

Hata watu wa visiwani wanaofanya hivyo pia hupigwa.Ni
wazi kwamba katika wakati huu ambapo siasa zimewagawa watu, kama kipo
kitu unachoweza kusema kimekuwa siku zote kikiwaunganisha Wazanzibari
basi ni wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Unapokuja mwezi mtukufu wa Ramadhani watu wa Zanzibar wana msemo kama ule wa manahodha
usemao, “hii ni meli yangu na sheria zangu zifuatwe” na kwa Ramadhani
watu wa Zanzibar wanasema, “hii ni nchi yangu na amri zangu zifuatwe.”

Tushirikianena wakati kila mmoja anaendelea kuwa na uhuru wa kuabudu dini aitakayo,
sio vyema kufanya jambo litalomuudhi muumini wa dini nyingine.

Waislamuna Wakristo kwa miaka nenda, miaka rudi Tanzania Bara na Visiwani
wameishi kwa kupendana na kuheshimiana licha ya tofauti zao za kidini.
Ni vyema utamaduni huu ukaendelezwa.

Magazine

Author & Editor

Has laoreet percipitur ad. Vide interesset in mei, no his legimus verterem. Et nostrum imperdiet appellantur usu, mnesarchum referrentur id vim.