BREAKING NEWS-TAZAMA VIDEO YALIYOJIRI LOWASSA ALIPOKUA AKIHOJIWA NA POLISI #TazamaVideo

Lowasa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa leo amefika kwa  Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika  Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ambapo amefanyiwa  mahojiano.
Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita ambapo wakati anaitwa hakupewa  maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo
Ingawa CHADEMA walitoa  maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.
Taarifa za awali zilionesha kuwa  kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.

Lowassa aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa hakuwa akijua  anachoitiwa, lakini akasema anahisi  ni kutokana na ushauri alioutoa kwa Rais Magufuli kumtaka  awaachie huru viongozi wa jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya kiislamu Zanzibar (Jumiki), waliokamatwa tangu mwaka 2012.

Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo jijini Dar es salaam alipozungumza katika futari iliyoandaliwa  na Mbunge wa Ukonga (Chadema) Mwita Waitara.

”Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho (leo) saa nne asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiita nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema juu ya masheikh wa Uamsho,” amesema Lowassa.

”Nilisema hivyo kwa sababu kuna Sheikh wakati wa kunikaribisha alisema japo tunasherekea Eid el Fitr bado kuna masheik wenzetu wanateseka. Nilisema hivyo kwa sababu nilishaahidi kwenye kampeni zangu kwamba tukishinda tutawatoa hao masheikh,” amesema Lowassa.
Robert Boaz, ambaye ni DCI amesema swala hilo aulizwe msemaji wa jeshi la Polisi, Advera Bulimba, ambaye pia kwa upande wake alisema hilo swala mzungumzaji mkuu awe Lowassa mwenyewe.

UPDATES KUTOKA KITUO CHA POLISI.
Mjumbe wa kamati kuu na mgombea urais mwaka 2015 ndugu Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya Polisi saa nne kama alivyoambiwa na DCI.
Lowassa alikuwa amefuatana na Magari manne ya kwake pamoja na magari mawili ya polisi wenye Siraha.
Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Mashinji. Aliwasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika.
Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa.
Kwa lolote litakalotokea tutazidi kujuzana.
Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.
Video tazama hapo chini

Magazine

Author & Editor

Has laoreet percipitur ad. Vide interesset in mei, no his legimus verterem. Et nostrum imperdiet appellantur usu, mnesarchum referrentur id vim.